Pages

Wednesday, 5 August 2015

[amakurunamateka.com] Tanzania: Kikwete aweka historia Chuo Kikuu Australia

 


RAIS Jakaya Kikwete ametunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria na Chuo Kikuu cha Newcastle cha nchini Australia, akiwa mkuu wa kwanza wa nchi kutunukiwa shahada hiyo chuoni hapo.Sherehe za kumtunuku Rais shahada hiyo zilifanyika jana katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Newcastle.


Akisoma maelezo ya utangulizi katika hafla hiyo, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle, Paul Jeans alisema Rais Kikwete ametunukiwa shahada hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika kuleta mabadiliko chanya.

Mabadiliko hayo si kwa Tanzania tu bali kwa dunia nzima kwani mchango wake umetambulika na mashirika mbalimbali ya kimataifa yakiwemo Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Benki ya Dunia kwa ujumla.

"Tangu kuingia madarakani Rais Kikwete amechangia katika kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu, uchumi na afya," alisema Jean na kuongeza: "Utawala wake umekithibitishia sio Chuo cha Newcastle pekee bali pia kuonesha kanuni ya Msingi kuwa Elimu ni muhimu katika kukuza uchumi, uvumbuzi na katika maendeleo ya jamii."

Tanzania imekuwa ikipokea misaada ya elimu kutoka Australia katika nyanja mbalimbali zikiwemo za madini, fedha, habari na tafiti mbalimbali ambazo zimeleta mabadiliko chanya katika jamii na duniani kwa ujumla. Kwa sasa Watanzania wanne wanachukua masomo ya uzamivu katika masuala ya elimu na siasa.

Tayari Watanzania 45 wamemaliza shahada na pia wapo watafiti kutoka Newcastle wanaofanya tafiti zao nchini Tanzania katika masuala ya elimu, afya na uhandisi. Rais Kikwete ameshukuru na kuelezea jinsi alivyoguswa na tukio hilo ambapo ameushukuru uongozi wa chuo hicho kwa kutambua mchango wake ambao ameelezea kuwa ameufanya wakati wa kipindi cha uongozi wake kwa moyo, upendo na nia njema kwa wananchi wote wa Tanzania na Dunia kwa ujumla.

Katika utawala wake Rais Kikwete ametunukiwa shahada za heshima kutoka vyuo mbalimbali vya Marekani, Canada, China, Uturuki na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Rais Kikwete pia ametunukiwa tuzo za heshima mbalimbali katika masuala ya Kijamii ya Umoja wa Mataifa, Afya, Technolojia na Maendeleo, nyingine ikiwa ya Demokrasia aliyoipata Uholanzi.

Rais pia amepata kutunukiwa na kutambuliwa kwa Mchango wake ambapo alitunukiwa nishani kadhaa za juu katika nchi za Uganda, Comoros, Saudi Arabia, Jamaica, Oman na nyingine. Rais Kikwete aliyekuwa na ziara ya siku nne nchini hapa, anarejea Dar es Salaam leo.



###
"Hate Cannot Drive Out Hate. Only Love Can Do That", Dr. Martin Luther King.
###

__._,_.___

Posted by: Nzinink <nzinink@yahoo.com>
Reply via web post Reply to sender Reply to group Start a New Topic Messages in this topic (1)
-------------------------------------------------------------------___________________________________________________
-Ce dont jai le plus peur, cest des gens qui croient que, du jour  au lendemain, on peut prendre une société, lui tordre le cou et en faire une autre.
-The hate of men will pass, and dictators die, and the power they took from the people will return to the people. And so long as men die, liberty will never perish.
-I have loved justice and hated iniquity: therefore I die in exile.
-The price good men pay for indifference to public affairs is to be ruled by evil men.
=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-=--=-=-=-=-=-=-=-=-=-=-
-To post a message: amakurunamateka@yahoogroups.com; .To join: amakurunamateka-subscribe@yahoogroups.com; -To unsubscribe from this group,send an email to:
amakurunamateka-unsubscribe@yahoogroups.com
_____________________________________________________
-More news:  http://www.amakurunamateka.com

https://www.facebook.com/amakurunamateka

https://www.facebook.com/musabeforum

http://www.musabe.com/
--------------------------------------------------------------------------------------
-SVP, considérer  environnement   avant toute  impression de  cet e-mail ou les pièces jointes.
======
-Please consider the environment before printing this email or any attachments.
--------------------------------------------------------------------------------------

.

__,_._,___

No comments:

Post a Comment

-“The root cause of the Rwandan tragedy of 1994 is the long and past historical ethnic dominance of one minority ethnic group to the other majority ethnic group. Ignoring this reality is giving a black cheque for the Rwandan people’s future and deepening resentment, hostility and hatred between the two groups.”

-« Ce dont j’ai le plus peur, c’est des gens qui croient que, du jour au lendemain, on peut prendre une société, lui tordre le cou et en faire une autre ».

-“The hate of men will pass, and dictators die, and the power they took from the people will return to the people. And so long as men die, liberty will never perish.”

-“I have loved justice and hated iniquity: therefore I die in exile.

-“The price good men pay for indifference to public affairs is to be ruled by evil men.”

READ MORE RECENT NEWS AND OPINIONS

Popular Posts

WebMD Health Channel - Sex & Relationships

Love Lectures

How We Made It In Africa – Insight into business in Africa

David DeAngelo - Dating Questions For Men

Christian Carter - Dating Questions For Women

Women - The Huffington Post

Recent Articles About Effective Communication Skills and Self Development